Kufuatia habari
iliyotoka juzi baada ya kuandikwa na gazeti moja la udaku na baadaye
kusambaa mitandaoni kuwa muigizaji maarufu nchini Wastara Juma Sajuki
anafikiria kuolewa ikiwa ni takribani mwaka na miezi kadhaa tangu
aliyekuwa mume wake na star wa filamu pia Juma Kilowoko(Sajuki) kufariki
dunia, muigizaji huyo amefunguka ya moyoni mwake kupitia page yake ya
facebook akionekana hana mpango wa kuolewa leo au kesho bali Sajuki bado
yupo moyoni mwake. Star huyo wa filamu za Vivian, Mboni Yangu, Kivuli
na Vita aliandika hivi jana katika page yake "Milele uko ndani ya
moyo.wangu kokote niendako nipo nawe ni kazi sana kuziba pengo langu,
nakupenda ni wewe tu Haupo kimwili lakini umeondoka na umeondoka na nusu
ya akili yangu huku hakuna linalofanyika bila kuvuta taswira yako
nakupenda sana Sajuki