Jamal Malinzi
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera, Jamal Malinzi amechaguliwa
kuwa Rais Mpya wa shirikisho la soka nchini, TFF
Kati ya 1999 na 2005, Malinzi alishika nyadhifa mbalimbali Yanga zikiwemo seneta, mkurugenzi wa kuchaguliwa, kaimu katibu mtendaji na katibu mkuu. Amekuwa mwenyekiti wa mashindano ya mpira wa miguu mkoa wa Pwani (2009 – 2011) na mjumbe wa Baraza la Michezo la Mkoa wa Dar es Salaam (2009-2012).
Toka 2011 hadi sasa ni mjumbe kwenye Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Misenyi, pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Kagera.