WASTARA ATONGOZWA KWA KIOO

MWENDELEZO wa kukupa vitu vipya kila siku, Amani  leo linakuletea kolamu mpya ya Kali Hazikuandikwa.
Hapa tutakuwa tunakuletea stori kali ya msanii ambayo ilitokea miaka ya nyuma lakini haikuwahi kuandikwa mahali popote.
Leo tunaanza na mwigizaji Wastara Juma Issa Abeid ‘Wastara’ na Haji Adam ‘Baba Haji’.
Wastara Juma.
Wastara ‘amefukunyua’ siri kwamba kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu.
Wastara aliweka bayana kuwa marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa mara ya kwanza.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo.
“Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana.
“Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu.
back to top