Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda kuwa ndiye aliyewaua Steven Kanumba na Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’.
Mbali na kudai kumuua Kanumba na Sharo, Mchungaji Mayanga alidai
kabla ya kuokoka kuwa alihusika na vifo vya watu milioni 605 wakiwemo
wasanii wa Kundi la Five Stars wapatao 14 na mwanamuziki James Dandu
‘Mtoto wa Dandu’ kwa njia za kichawi.Mara baada ya gazeti la Amani toleo namba 782 la Oktoba 17, mwaka huu kuripoti habari hiyo, mama Kanumba alipelekewa nakala yake nyumbani ambapo baada ya kuisoma, ndipo alipoona kuna kila sababu ya mchungaji huyo kukamatwa kwa kuwa atakuwa amehusika moja kwa moja na kifo cha mwanaye Kanumba. “Mama Kanumba alipata mshtuko mkubwa siku ile alipoliona lile gazeti, maskini alikuwa tayari ameanza kusahau machungu ya kuondokewa na mwanaye,” kilisema chanzo kilicho karibu na mama Kanumba.
Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa.
Mara baada ya chanzo hicho kupenyeza habari hizo, paparazi wetu
alimtafuta mama Kanumba ili kumuuliza alipokeaje habari za mchungaji
huyo ambapo alipopatikana, alitiririka; “Naiomba serikali imkamate huyo
mchungaji, maana yeye si amesema amemuua mwanangu, sasa iweje aendelee
kutanua mtaani wakati ameweka wazi kuwa amemuua mwanangu. “Imeniuma
sana, ameamsha machungu ambayo tayari nilianza kuyasahau. Huyo mchungaji
akamatwe na sheria imchukulie hatua stahiki,” alisema mama Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba.
Hata hivyo, katika ushuhuda alioutoa mchungaji huyo, alijitabiria
kuwa ipo siku atakamatwa na kufungwa kutokana na siri za vigogo ambao
aliwapa utajiri kwa nguvu za giza. “Nina siri za watu wengi sana,
nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu
watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe
siogopi kwa kuwa Bwana ameniongoza,” alisema.Juzi gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta mama Sharo Milionea, Zainabu Mkiete lakini hakupatikana kwani simu yake iliita bila ya kupokelewa. Mchungaji huyo alipotafutwa naye simu yake iliita bila kupokelewa.