WANAWAKE NCHINI SAUDI ARABIA KUANDAMANA KUPIGA SHERIA YA MWANAMKE KUTORUHUSIWA KUENDESHA GARI NCHINI HUMO
Leo October 26 2013 ndio Wanawake
nchini Saudi Arabia wamepanga kuandamana kupinga wao kunyimwa kuendesha
magari sehemu yoyote nchini humo ikiwa ni nchi pekee duniani ambayo
inakataza Wanawake kuendesha magari hata kama wanaweza.
Unaambiwa kwa sasa Mamlaka za Saudi
Arabia zimewaonya Wanawake hao kutoandamana katika maandamano hayo
yatakayokua ya aina yake na ya tatu kutokea nchini humo toka mwaka 1990
ambapo Wanawake kadhaa walikamatwa na wengine kuachishwa kazi, onyo hilo
linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote ambae amepanga kuendesha gari
Msemaji wa Serikali amesema Mwanamke
yoyote atakae endesha gari leo atachukuliwa hatua za kisheria ambapo
wakati siku hii ya kuandamana ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia
tayari walishaweka video zao wakiendesha magari sehemu mbalimbali za
Saudia lakini mpaka sasa hawajakamatwa.
Mpaka sasa zaidi ya watu elfu 17
wamesain kura ya ndio itakayo waruhusu Wanawake wa Saudi kuendesha
magari ambapo pia idadi ya Wanaume wanaosupport imeendelea kuongezeka
kwa kasi.