Ofisa wa polisi akiwazuia wanahabari (hawapo pichani) kuingia katika uchaguzi wa TFF.
Wanahabari wakirumbana na polisi baada ya kuzuiliwa.
Mmoja wa wagombea (kushoto) akiwatuliza wanahabari.
WAANDISHI wa habari leo walizuiliwa kuingia kwenye uchaguzi wa
viongozi mbalimbali unaofanyika katika Ukumbi wa Water Front jijini Dar
es Salaam.Mkurugenzi wa kamati ya uchaguzi huo, Hamidu Mbwelezeni alisema waandishi hawaruhusiwi kuingia kwenye uchaguzi huo mpaka saa 1 usiku yatakapotangazwa matokeo ndipo wataruhusiwa kuingia.
Hali hiyo ilizua mtafaruku baada ya wanahabari kusema kuwa utaratibu huo haujawahi kutokea kwani chaguzi zote huwa wanashiriki mwanzo mpaka mwisho. Wanahabari hao waliongeza kuwa, huenda kuna kitu wanafichwa kuhusu uchaguzi huo. Wanahabari hao walizuiliwa nje ya jengo hilo tangu saa 3 asubuhi.
( GPL)