KIM KARDASHIAN ANG’ARA KATIKA GAUNI JEUPE BETHIDEI YAKE HUKO LAS VEGAS

 
Kardashian akiwa katika pozi tofauti na gauni lenye mvuto wa kike. Picha hizi alizitupia katika akaunti yake ya Instagram.
Kim Kardashian akipozi na mpenzi wake Kanye West.
STAA Kim Kardashian alikuwa na kila sababu ya kusherehekea usiku wa kuamkia jana wakati wa kuadhimisha mwaka wa 33 wa kuzaliwa kwake huko Las Vegas, Marekani.  Shamrashamra hizo zilikuwa ni pamoja na kuchumbiwa rasmi na mwanamuziki Kanye West wiki iliyopita, na furaha ya kupata mwanaye aitwaye Nori mwezi Juni mwaka huu.
Kardashian aliiweka picha hii katika akaunti yake ya Instagram baada ya kufika Sin City.
back to top