TATHMINI: HAWA NDIO MARAIS WANAOLIPWA PESA NYINGI ZAIDI DUNIANI, RAIS JAKAYA KIKWETE KAWAIDA SAAANA...!

Rais wa Marekani analipwa Dola 400,000 (Sh 640 milioni) kwa mwaka, sawa na Sh 53.3 milioni kwa mwezi. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma analipwa Randi 2 ,917 038 sawa na zaidi ya Sh400 milioni za Kitanzania kwa mwaka, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande Sh475 milioni, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Sh338 milioni, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Sh277 milioni na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba Sh226 milioni kwa mwaka. Wengine na malipo wanayopata kwa mwaka ni Marais wa Urusi, Vladimir Putin, Sh174 milioni,
Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia Sh137 milioni, Michael Satta wa Zambia, Sh126 milioni, Rais wa Angola, Jose dos Santos Sh91 milioni, Rais wa Lesotho, Profesa Pakalitha Mosisili Sh88 milioni, Armando Guebuza wa Msumbiji, Sh84 milioni na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping Sh60 milioni. Wengine ni Rais wa India, Pranab Mukherjee Sh49 milioni, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Sh27 milioni, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Mothlanthe Sh331 milioni,
Waziri Mkuu wa Namibia, Nahas Angula Sh160 milioni.

Ok kumbe Mshahara wa Rais wa bongo bado ni mdogo sana kulinganisha na mishahara ya Marais wenzake hapa Africa na Duniani, Mheshimiwa Zitto my hero kwenye hili hakumtendea haki Rais wetu alipotoa hadharani Mshahara wa Rais wetu ambayo nia na madhumuni yake ilikuwa kuonyesha kwamba analipwa mahela mengi sana, alitakiwa kutuonyesha pia na mishahara ya Marais wengine na vipato vya Taifa pia, kwa sababu as a nation tuna pato kubwa sana kuliko nchi nyingi zingine ambazo Marais wao wanalipwa mahela ya ajabu kulinganisha na Rais wa bongo.

Pia ifahamike wazi kwamba hata leo Rais wa Jamhuri akitokea Chadema, bado mshahara wake utakuwa ni huo huo unless akigoma na kutaka upunguzwe, kitu ambacho historia ya chama hicho na Mishahara au posho za Taifa haiko kabisa upande wao, kuna wakati walidai posho ya wabunge ni kubwa sana lakini mpaka leo hatujasikia wakiomba kupunguziwa, walilalamika kuhusu hela za magari ya wabunge lakini mpaka leo hawajagomea kupokea hela hizo, Mwenyekiti wao alilalamikia magari ya kifahari ya wabunge na yeye mpaka leo anatumia gari hilo hilo alilolalamikia!
 
-Wiliam Malecela
back to top