NEY WA MITEGO AWEKWA SERO KWA KOSA LA KUTUMIA SARE ZA POLISI KWENYE VIDEO YAKE BILA KIBALI....
Rapper
Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea
Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa
kwenye radio stations ' Salam Zao'.
Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilituwa sero
jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu
kwasababu kulikuwa na waigizaji
waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani
nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia
sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu
kilichopelekea nikapelekwa polisi.
Mitego
ameendelea kusema kuwa baada ya kukaa sero kwa dakika kama 15 mkuu wa
kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya
kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuoneknaA uraiani.
Ney aliwekwa sero Kwenye kituo
cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana
kwenye vituo vya televison Tanzania.