MWANAMUZIKI MOHOMBI NZASI AWASILI JIJINI DAR

 
Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo (kulia) akifanya mahojiano na wanahabari baada ya kutoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kufanya shoo kali ya Serengeti Fiesta inayotegemea kufanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club. 
Mohombi (kulia) akisindikizwa kutoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kushuka na ndege ya Turkish Air Lines na Afisa wa ndege hiyo Ebubekir Ekici ambaye pia alifurahia ujio wake Tanzania.
 
Msanii wa kimataifa anayetamba na kibao chake kikali cha “Kiss Me” akiwa amepozi na mtangazaji wa Clouds TV baada ya kupokelewa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 
Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya shoo kali ya Serengeti Fiesta itakayofanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club. Mbele yake ni Fauzia mratibu wa shughuli za Serengeti Fiesta kutoka Prime Time Promotions.
back to top