MTANGAZAJI wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka na Weekly Star Exclusive na kuanika kuwa tangu amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kuanguka dhambini na mwanaume mwingine.
Nasibu Abdul na Jokate Mwegelo.
Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka
jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenzi wake, mcheza kikapu
wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit.Akizidi ‘kutema madini’ mbele ya kinasa sauti cha Weekly Star Exclusive, Jokate alisema kwa kuwa alikuwa na mapenzi ya dhati na Hasheem, ndiyo maana alimwagana na Diamond ndani ya muda mfupi na tokea hapo amekuwa bize na kazi zake.
“Daah! Nipo bize sana na kazi zangu, ninaimba, ninaigiza, nina kampuni yangu ya urembo ya Kidoti huku bado natakiwa kutangaza Channel O basi kazi kwelikweli hata muda wa huyo mwanaume nakosa,” alisema Jokate.
Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya kibaiolojia, Jokate alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi.
“Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema.