Askari
wa Mgambo wa Kijiji cha Lwande Wilayani hapa, Salum Mgonje amekufa kwa
kushambuliwa na mapanga na kundi la watuwaliokuwa wakipinga kitendo cha
mwenzao kulipishwa ushuru wa manunuzi ya zao la hiliki wa Serikali ya
Kijiji.
Mashambulizi hayo baadaye
yalizusha mapigano baina ya kundi la watu waliokuwa wakimsaidia
mfanyabiashara huyo na askari wa jeshi la polisi walipokwenda kuwakamata
waliohusika na mauaji ya mgambo.
Katika mapigano hayo,Mkuu wa
Kituo cha Polisi cha Kilindi Edward Lusekelo, ambaye aliongoza askari
waliokwenda kuwakamata wahusika na mauaji ya Mgambo alijeruhiwa kwa
kupigwa risasi kwa bunduki ya ShortGun.
Kwa mujibu wa habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamnada wa Polisi wa Mkoa wa
Tanga,Constantine Massawe, zilithibitisha kuwa askari wa
mgambo mmoja aliuawa juzi mchana katika tukio hilo lililotokea katika
kijiji cha Lwande, huku Mkuu wa kituo akijeruhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya
Kilindi,Selemani Liwowa alisema chanzo cha mapigano hayo ni
mfanyabiashara huyo kutoka Kijiji cha Lulago Kata ya Lwande kwenda
Kijiji cha Lwande kununua hiliki ambapo baada ya kukaidi kulipa ushuru
mgambo alilazimika kumtia msukosuko ili aweze kulipa kama ilivyo sheria
ya kijiji.
Ndiyo chanzo cha kutokea kwa
vurugu hizo baina mgambo na wafanyabiashara ambapo baadaye
walimshambulia kwa mapanga na kisha kumuua.
Aidha, alisema taarifa za mauaji
ya mgambo zilizpofika kituo cha Polisi ilimlazimu mkuu wa kituo kuongoza
kikosi kilichokwenda kijiji cha Lwande kwa ajili ya kuwasaka
waliohusika na baada ya kuwasili kijijini hapo likajitokeza kundi la
watu wenye silaha na kuanza kuwashambulia askari hao jambo
lililosababisha askari hao kujibu mashambulizi.
Akithibitisha
habari hizi,Kamanda Massawe alisema tayari watu wanne wanashikiliwa na
jeshi la Polisi kwa kuhusika na tukio hilo huku mkuu wa kituo cha
Polisi akiwa amekimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo kwa
ajili matibabu
chanzo; http://habarizetuleo.blogspot.com