AUAWA KWA KUIBA KUKU WATATU!

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Frank William Shoka (30) mkazi wa Kitongoji cha Katusi, Kijiji cha Mjere, Wilaya ya Mbeya vijijini mkoni hapa ameuawa kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid.

 
Kuku walioibiwa.
Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20, mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manani na kuchukua kuku hao wakati yeye akiwa hayupo.
Aidha, Dismas alisema baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa nao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya na alipomuuliza juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Hata hivyo, baada ya marehemu Shoka kushindwa kutoa maelezo sahihi juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga mazingira yaliyomfanya apoteze maisha.
 
Ndugu wakiwa na mwili wa marehemu.
NDUGU WAKAA NA MAITI KWA SAA NANE!
Hata hivyo, baada ya tukio hilo hakuna mwananchi hata mmoja aliyediriki kukaa na maiti hiyo isipokuwa ndugu wake ambao walikaa na marehemu kwa muda usiopungua saa nane.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho, Evarist Benny ambaye alitoa taarifa Kituo cha Polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi na  Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.

MMOJA WA KUKU WALIIBIWA ATAGA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati polisi wanakamilisha taratibu na kumkabidhi marehemu kwa ndugu,   mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai jambo lililozua mshangao miongoni mwa mashuhuda.

KUTOKA IJUMAA:
Si jambo jema hata bkidogo kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi, kwani sheria zipo ili zifuatwe na kama mtu amekwenda kinyume cha sheria hizo basi afikishwe kwenye vyombo vinavyohusika na sheria itachukua mkondo wake- Mhariri.
back to top