Tamrina Poshi ‘Amanda’
Akichonga na paparazi wetu muda mchache baada ya wadau kibao kumtaka
mwanadada huyo arudiane na mpenzi wake huyo kupitia mtandao wa kijamii
wa Facebook, Amanda alisema tayari ameshapenda kwingine hivyo hapendi
kumzungumzia mtu aliyeachana naye pia hana tabia ya kurudia matapishi
yake.“Siwezi kurudiana na Misosi kwani nikishaachana na mtu basi ninamtoa moyoni mpaka mdomoni nikiwa na maana sina muda wa kukaa na kumzungumzia ndiyo maana hata wadau waliokuwa wakinitaka nirudiane naye sijawajibu chochote,”alisema Amanda.