
Luis Suarez akiwa mwenyewe kwenye uwanja wa mazoezi wa Liverpool huko Melwood.
Kocha
wa klabu ya Liverpool Brendan Rogers amemuamuru mshambuliaji wa klabu
hiyo Luis Suarez kufanya mazoezi mwenyewe ikiwa ni hatua ya kinidhamu
kwa mshambuliaji huyo kwa kitendo ambacho kocha wake alikiita kuikosea
Liverpool heshima .
Rogers
amechukua hatua hiyo baada ya Suarez kuzungumza na vyombo vya habari
ambapo alisema kuwa klabu yake ilimuahidi kumuuza endapo ingeshindwa
kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa ahadi ambayo Liverpool wanaonekana
kuivunja .
Sakata
linalohusu mustakabali wa mshambuliaji huyo ndani ya Liverpool linazidi
kuwa gumu kadri siku zinavyoenda na kwa sasa wakala wa mshambuliaji
huyo amekuwa akihangaika kulazimisha kuondoka kwake huku klabu ya
Arsenal ikiwa inataka kumsajili.

Kocha wa Liverpool Brendan Rogers amemuadhibu Suarez kwa kumtaka afanye mazoezi mwenyewe.
Suarez alizungumza na
vyombo vya habari siku ya jumatatu ambapo alifunguka na kusema kuwa
Liverpool iliahidi kumuuza kama ingeshindwa kufuzu michuano ya ligi ya
mabingwa barani ulaya .
Hata hivyo imegundulika
kuwa kipengele ambacho kipo kwenye mkataba wa Suare z ambacho wakala wa
mchezaji huyo na mchezaji mwenyewe walidhani kinatoa ruhusa ya kuuzwa
kwa klabu yoyote ambayo itafikia bei ya paundi milioni 40 hakiko kama
walivyodhani na badala yake kinasema kuwa endapo itajitokeza klabu yenye
nia ya kumnunua Suarez klabu itamtaarifu kuwa kuna klabu inamtaka
pasipo kulazimika kumuuza .
Wakala wa Luis Suarez
ambaye ni mdogo wa kocha wa Barcelona Pere Guardiola amekuwa akihangaika
na wanasheria toka Hispania kubadilisha kipengele hicho ili kutoa fursa
kwa Suarez kuuzwa .
Kesi hiyo huenda
ikahamia kwa viongozi wa ligi kuu ya England na umoja wa wachezaji PFA
ambao wamekuwa wakifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu.