MWANAMUZIKI Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye alikuwa hoi kwa madawa ya
kulevya, juzikati ametupia maneno ya faraja kwenye mtandao wa Instagram
akieleza kuwa amekuwa akipewa mitihani migumu katika maisha yake lakini
kwa uwezo wake Mungu amekuwa akishinda.
Ray
C anayetarajia kurejea kwenye ‘game’ hivi karibuni, akasema anaamini
yeye ni msichana imara kutokana na namna alivyokuwa akipambana na sasa
ni Ray C mpya.
Aliandika hivi: “The New Ray C, am strong lady (Ray C mpya, mimi ni
msichana imara)…kila nipewapo mtihani mgumu wa maisha napigana mpaka
nakuwa mshindi.”
Pia kupitia mtandao huo, Ray C alitupia video ambayo anasikika
akiimba wimbo wa msanii wa THT,Winfrida Josephat ’Recho’ uitwao Upepo
kisha akaandika: “I love your voice my sis.” Recho akajibu: Thanks a lot
my dada.”