
Boaz alisema kuwa baba wa kijana huyo ndiyo aliyemfumania kwa kuwa alikuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na ndipo alipomkamata.
Alisema kuwa kabla ya tukio hilo kijana huyo aliwahi kukutwa akifanya mapenzi na kuku na kuanzia hapo mzazi wake huyo akaanza kumfuatilia na hivyo kumkamata akifanya mapenzi na ng’ombe ambaye ni ndama.
Kamanda alisema kuwa baada ya kukamatwa kijana huyo alifikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa ambapo alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa amekuwa akitafuta wasichana bila mafanikio.
Aidha aliongeza kuwa kila msichana anayemtakia neno la mapenzi amekuwa akitaka fedha nyingi wakati yeye ni mwanafunzi hana uwezo wa kupata fedha.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana huyo alishapata taarifa siku za nyuma kuhusiana na tabia ya kijana wake huyo na ndipo akaanza kumfuatilia na kwa sasa anashikiliwa na polisi uchunguzi zaidi ukiendelea.