BATULI AANZA KUTEMBELEA MAGONGO BAADA YA KUUMIA AKIWA ANATENGENEZA FILAMU... !!
MSANII wa filamu nchini Zaytun Kibwana , 'Batuli' sasa atembelea magongo
baada ya kupata matibabu ya mguu baada ya kuumia akiwa anatengeneza
filamu 'Location'.Msanii huyo ambaye anashindwa kutembea au
kujisogeza ameweza kupata matibabu kwa kuwekewa kifaa maalumu,
kitakachoweza kurudisha goti katika hali ya kawaida. Akizungumza mara
baada ya kuwekewa kifaa hicho chenye chuma, Batuli aliweka wazi kuwa
ameanza kupata nafuu ingawa anatumia magongo kwa ajili ya kutembea na
kusimama.
Alisema dokta ndiye aliyemshauri kutumia kifaa hicho
kuliko kufanya upasuaji ambao ungempelekea kukaa kitandani kwa muda
mrefu huku akishindwa kutembea.
"##Sasa namshukuru mungu naendelea
vizuri ingawa siwezi kutembea wala kusimama hivyo inanilazimu nitumie
magongo, nimeweka kifaa hicho mguuni naamini nitapata nafuu muda si
mrefu" alisema Batuli.
Alisema gharama za hospitali ni kubwa hali
iliyopelekea ashindwe kumudu pekee yake hali iliyosababisha aombe
msaada kwa baadhi ya ndugu wanaomzunguka ili aweze kujitibu.
Batuli
anasumbuliwa na mguu huo kwa muda mrefu, lakini umezidi baada ya
kushtuka tena alipokuwa location hali iliyomsababisha kushindwa kutembea
au kujisogeza.