Baada ya Feza Kessy na Ammy Nando kutoka kwenye jumba la BBA, nafasi yao
kuongeza figures kwenye bank account zao kutokana na mashindano haya
bado ipo. Unaambiwa
mmoja kati ya Big
brother housemates atachaguliwa kuwa brand ambassador wa kampuni ya RLG
communications ambao ni wauzaji wa Uhuru tables na pia ni co-sponsor
wa BBA The Chase.
RLG communications wamekua wanatoa zawadi za tablets kwa watu
wanaowapiga kura kwa washiriki wa Big brother, lakini mpango wao hivi
sasa ni kumchagua mmoja kati ya washiriki wa BBA The Chase kuwa brand
ambassador. Feza na Nando bado wana nafasi ya kupata hili dili.