Arsenal waelekea kumkosa Gustavo.

image
Hii ni taarifa ambayo mashabiki wa Arsenal hawataipokea vizuri hasa ukizingatia kuwa ni kitendo ambacho kitakuwa kinatokea kwa mara ya pili katika kipindi hiki cha dirisha la usajili kuwa wazi.
Taarifa toka nchini Ujerumani ambazo zimeripotiwa kwenye gazeti moja la jioni linalofahamika kwa jina la Welte zinasema kuwa kiungo wa kimataifa wa Brazil Luiz Gustavo amekubali kujiunga na klabu ya Bundesliga ya Wolfsburg .

Awali kulikuwa na taarifa za kuthibitika kuwa kiungo huyo alikuwa karibu kujiunga na Arsenal baada ya klabu yake ya Bayern Munich kuikubali ofa ya Arsenal ya Euro Milioni 19 kwa ajili ya kumnunua .
Wolfsburg ndio ilikuwa timu ya kwanza kufanya jitihada za kumsajili Luiz Gustavo baada ya mchezaji huyo kuwekwa kwenye Orodha ya wachezaji watakaouzwa kwa kuwa hayupo kwenye mipango ya kocha Pep Guardiola .
image
Gustavo mwenyewe aliripotiwa kuvutiwa na uwezekano wa kujiunga na Arsenal na taarifa za kujiunga na Wolfsburg zitakuwa zimewaumiza mashabiki wa klabu hiyo ambao kwa muda mrefu walikuwa wanajipoza kwa kumkosa mshambuliaji Gonzalo Higuain ambaye alikuwa karibu kujiunga na klabu hiyo (Arsenal) toka Real Madrid kabla ya kubadili mawazo na kuhamia Napoli.
back to top