Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe baada ya kuanguka.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio hilo
lilijiri kwenye Ukumbi wa PG Hall (zamani FM Club), Kinondoni jijini Dar
ambapo mastaa kibao walihudhuria.Ndani ya kibao kata hicho, Wolper alicharuka kipombepombe kwa kucheza ovyo na kukimbiakimbia akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga mwereka na kuanguka huku akijaribu kusimama kwa kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Mbali na pombe pia alikuwa kivutio kwa staili ya ukataji wake wa mauno akiwa na kivazi kilichoacha nje mapaja yake akiwa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.
Katika hatua nyingine, Vanita alijikuta akiangua kilio baada ya wapiga ngoma wa kibao kata ‘kuwa feki’ na kushindwa kufanya kazi kama walivyoahidi.
Mshereheshaji akimvaa Vanita.
Kutokana na hilo, baadhi ya mastaa kama Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf
‘Batuli’ waligoma kucheza na kukizomea kibao kata hicho ambacho
kililetwa na MC (jina linahifadhiwa) akidai kuwa amewatoa Bagamoyo na
wana ufundi wa hali ya juu.