WENGER NI KIBONDE WA MILELE WA JOSE MOURINHO, HAKUNA UBISHI

USIJALI sana Arsene – bila shaka itakuwa bahati ya mara ya 10 wakati Jose Mourinho na timu yake, Chelsea watakapokwenda Uwanja wa Emirates Jumatatu ya Desemba 23, mwaka huu.
Kipigo cha Arsenal cha mabao 2-0 katika Kombe la Ligi maarufu kama Capital One kutoka kwa Chelsea usiku wa jana ilikuwa ni mara ya tisa Wenger anakutana na Mourinho na kutoka kichwa chini.
Rekodi yake dhidi ya Mreno huyo inamaanisha yeye ni mnyonge: amefungwa mara tano na kutoa sare nne. Anapotokea Mourinho, Wenger ni kibonde sana.

Ubabe pale pale: Ushindi wa Chelsea kwa Arsenal unamfanya Jose Mourinho aendeleze rekodi ya kutofungwa na Arsenal Wenger (chini)

<<KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA FORUM YETU>>
back to top