Umeipata kauli ya Tanzania kuhusu kutengwa na Rwanda, Kenya na Uganda?

Rwanda 
Tanzania imetoa wiki mbili kwa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililo chini ya Uenyekiti wa nchi ya Uganda kutoa taarifa ya kina kuhusu mikutano inayoendeshwa na baadhi ya nchi sambamba na mikutano ya kawaida ya kalenda ya Jumuiya hii.

Hili agizo limesikika kutoka kwa waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta wakati akijibu maswali bungeni Dodoma October 30 2013 baada ya kuulizwa uhalali wa Tanzania kuendelea kubaki kwenye Jumuiya hii wakati inatengwa na nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.
Waziri Sitta amesema wakati Tanzania inasubiri ufafanuzi wa hoja yake, itaendelea na msimamo wake wa kutoyatambua maamuzi yote yanayojadiliwa na kuamuliwa nje ya utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
‘Kama wenzetu hawa wana hila haitochukua muda tutazibaini tu lakini kwa kuwa sisi tumeshamuhoji mwenyekiti wetu wa baraza la Mawaziri na baada ya wiki mbili tuna kikao… basi tusubiri tutakachoambiwa, kama utaendelea uongo wa kitoto Serikali hii ni makini tutakuja bungeni kuweka mapendekezo yatakayokabiliana na hali ya kuchezewachezewa’ – Sitta
Samwel_Sitta 
Baada ya hilo jibu, Mbunge wa Mbinga John Komba aliuliza kwanini na sisi tusiunde Jumuiya yetu mpya ya Tanzania, Burundi na Congo badala ya kuwabembeleza hawa marais wa ajabuajabu? swali hili lilijibiwa na Waziri Sitta kwa kusema ‘Nchi zetu hizi za Afrika mara nyingine matatizo yanaletwa tu na viongozi, mnaelewa kwanini Rwanda inatununia…. tusichukue hatua sasa ambazo zinajibu uchokozi flani matokeo yake sisi tuwe tumeharibu zaidi hiyo ndio sababu hatuchukui hatua ya kulaani hivi sasa lakini wakati wowote mambo yakidhihirika basi na hatua tutakayochukua ni hatua ya hekima yenye kulinda maslahi ya Tanzania’
Mikutano ya nchi za Uganda, Kenya na Rwanda bila kuishirikisha Tanzania ilianza kufanyika Entebbe Uganda June 24 2013 ambapo mkutano wa pili ulifanyika August 28 2013 kwa kigezo cha kuzindua gati kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya huku mwingine ukifanyika October 29 2013 Kigali Rwanda.
chanzo; http://millardayo.com
sou
back to top