Rihanna aingia tena kwenye headlines na tatoo nyingine mkononi

riri 
Watu ambao wameshawahi kuchora tatoo wanasimulia maumivu makali wakati wa kuchora tatoo hizo, lakini kwa upande wa Rihanna labda anapenda hayo maumivu makali ya kuchora tatoo. Hata miezi michache haijapita tangu achore tatoo huko New Zealand ambayo inasemekana ni moja kati ya tatoo inayokupa maumivu makali sana ukiwa unachora. Rihanna ameshaongeza mchoro mwingine juu ya hiyo tatoo.

Sources zinasema kwamba baadaya muda mfupi wa kuchora tatoo huko New Zealand, Rihanna hakuipenda tena ile tatoo. Mwimbaji huyo alimsafirisha mchora tatoo kutoka New York hadi Jamhuri ya Dominica ambapo Rihanna yupo kwenye tour. Kikubwa alichokifanya mchoraji huyo ni kuchora tatoo mpya juu ya tatoo ya zamani kama inavyoonekana hapo chini.
ne9q3n
2i7tyjk (1)