SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA DINI YENYE "VIRUSI" VYA UCHOCHEZI
Waziri wa MAmbo ya Ndani ya NChi, EMmanuel NChimbi, ameliagiza jeshi la
polisi kuanzia IGP, RPC, OCD na OCS kuwachukulia hatua wale wote
wanaoendesha mihadhara ya kidini yenye kuchochea vurugu na mifarakano
katika jamii. ...
Nchimbi amesema kuwa kiongozi yeyote ambaye atabainika kutochukua
hatua licha ya taarifa kuripotiwa kwake basi atakwenda na maji.. ...
Kauli hiyo ameitoa jijini dar es salaam jana wakati akiongea na wawakilishi wa
viongozi wa dini na vyombo jeshi la polisi mkoa wa dar es salaam
Waziri Nchimbi amewatahadhalisha vijana wanaoshinda kwenye mitandao
na wanaotumia simu kutuma ujumbe wenye lengo la kuhamasisha chuki za
kidini. Amesema kuwa kuanzia sasa serikali itachukua hatua
stahiki
Chanzo: taarifa ya habari ya TBC1 ( saa nne asubuhi)