BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA MWINGINE BAADA YA KUZINGUANA NA MUMEWE ....
MWIMBAJI wa Muziki wa Injili ,
Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo
linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa
talaka yake
Akizungumza na mwandishi wetu
jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia Haina
Huruma aliweka wazi kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata
mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa
yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
Bahati alisema kuwa kifuatacho
inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana
polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa
kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi
amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa
akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku
aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki
dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.