![]() |
Demba Ba
|
Mabingwa
watetezi Chelsea wameanza vyema utetezi wao kwa kuivurumisha Southampton
Bao 5-1 kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA Cup iliyochezwa nyumbani kwa
Southampton.
Aidha raund ya 3
ya FA CUP Januari 5,2013 imeshuhudia Timu za Ligi Kuu Uingereza Aston Villa,
Reading, Manchester City, Norwich,
Chelsea na Spurs zikisonga kuingia Raundi ya 4 huku Sunderland, Stoke, Fulham,
QPR, West Brom na Wigan zikiambulia sare na itabidi kucheza Mechi za marudiano
lakini Newcastle walipata aibu kwa kubwagwa nje walipofungwa 2-0 na Brighton
inayocheza Daraja la chini.