Mchungaji Rwakatare acharuka Bungeni! Ngoma za Vigodoro Chanzo
Akichangia
hoja ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Watoto
Bungeni leo; ameomba kwa uchungu, Watanzania kukemea ukeketaji, ngoma za
kudhalilisha kama vile kangamoko na Vigodoro na nyinginezo na upigaji
wa wanawake!
In
fact, inashangaza jinsi ngoma hizi za ovyo zinavyoshamiri Dar,
inashangaza ni kwanini serikali kupitia wizara hii hawakomeshi ngoma za
ovyo kama hizi! Kule Boko Beach kuna ngoma ya ovyo (Kigodoro) kabisa
huchezwa kila wikiendi, viongozi wa serikali ya mtaa hawaoni?