ARSENAL BINGWA FA, NI BAADA YA MIAKA 9 BILA KOMBE!
Arsenal
wametwaa kombe la FA baada ya kukaa miaka tisa bila kombe lolote.
Wametwaa ndoo hiyo kwa kuifunga Hull City bao 3-2 katika muda wa
nyongeza baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida kwenye Uwanja wa
Wembley usiku huu.
Wafungaji
Arsenal: Carzola dakika ya 17, Koscielny dakika ya 71 na Ramsey dakika
ya 109 wakati ya Hull City yakifungwa na Chester dakika ya 4 na Davies
dakika ya 8.