ISABELA: KALAMA AMENITULIZA

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda amekiri kuwa mpenzi wake, Luteni Kalama ndiye aliyemtuliza  mapepe aliyokuwa nayo.
Miss Ruvuma 2008, Isabella Mpanda ‘Bella’ na mchumba’ke ambaye ni memba wa Kundi la Gangwe Mob, Karama Bakari ‘Luteni Kalama’.
Akistorisha na safu hii, Isabela alisema kama siyo Kalama, asingekuwa na tabia njema.
“Amefanya kazi kubwa sana kunibadilisha, zamani nilikuwa mapepe kweli, kujirusha na skendo za ajabuajabu, lakini sasa nimeacha,” alisema.
back to top