HATARI SANA..MMMH...RAY C NA DIAMOND NINI KINAENDELEA NYUMA YA PAZIA?!!!FUATILIA ZAIDI HAPA...

 
Ray C
Msanii "kiuno bila mfupa" Rehema Chalamila. 'Ray C' anadaiwa kuwa bize na harakati za kumnasa sukari ya warembo Naseeb Abdul 'Diamond' katika anga za mazoezi huku duru za habari zikidai kuwa muda si mrefu kuanzia saaa yataandikwa mengi juu ya wawili hao.Mwandishi wetu alizungumza na rafiki wa karibu na Ray C hivi karibuni na kuambiwa kuwa muda mwingi jina la Diamond halikatiki mdomoni mwa mrembo huyo.
Diamond Platnumz
Chanzo chetu cha habari kilizidi kudai kuwa kwa sasa Ray C hana furaha hadi atakapotimiza nia na lengo la kumnasa Diamond hapo ndipo furaha yake itakapotimu

Aidha habari zinazidi kudai kuwa mara kadhaa Ray C amekuwa akipanga Miadi ya kukutana na Diamond licha yakushindikana kwa apointiment hizo kila mara "kwa sasa Ray C haambiwi kitu kwa Diamond, ana haha kila wakati kumweka mikononi mwake, hana furaha kabisa hadi lengo lake litakapotimia, na muda si mrefu mtaandika juu ya hao" alisema rafiki wa karibu wa Ray .
Wema Sepetu
Mwandishi wetu aliwatafuta wawili hao kwa njia ya simu ambapo simu ya Ray C ilionekana kuwa bize muda mwingi huku Diamond akidai kutokuwa na taarifa juu ya madai hao "kaka mimi sina taarifa kabisa na habari hizo, kwangu Ray C namchukulia kama dada yangu" alisema Diamond.
Mwandishi wetu alipomtaka Diamond kufafanua hatua atakayochukua endapo mrembo huyo ataamua kumwambia anamtaka ambapo kwa haraka Diamond alisema "NO COMNENT (sina cha kujibu)" na kukata simu.  

<<KUPATA HABARI ZAIDI ZA UDAKU BOFYA HAPA>> 

back to top