MSANII wa filamu Bongo, Kajala Masanja amewajia juu watu wanaomsema kuwa hajui kumlea mwanaye kutokana na mavazi mafupi anayomruhusu binti yake aitwaye Paula ayavae.
Mpango mzima ulitokea wiki iliyopita ambapo awali, Kajala aliweka
picha akiwa katika pozi mbalimbali na mwanaye huyo kwenye mtandao wa
Instagram ndipo wadau walipoanza kuchangia kuwa anamharibu mtoto wake
kwa kumruhusu kuvaa nguo fupi, jambo lililomfanya Kajala ajibu mapigo
kwa wafuasi hao mtandaoni.
“Nawashangaa sana watu wengine mnajifanya mnajua sana kuongea kuhusu mambo yasiyowahusu. Kuna mzazi yoyote anataka mwanaye apotee? Acheni mambo ya kishamba, unataka mtoto avae dira kwani yeye mtu mzima. Kama unaona namlea mtoto wangu vibaya niachie mwenyewe… zaa wa kwako umlee vizuri,” aliandika Kajala.
chanzo; GPL.