UTAFITI: HAYA NDIO MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA...

MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA
Katika moshi wa sigara, zaidi ya kemikali 400
zimegundulika kuwa na madhara makubwa
katika afya. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya
pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri
mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa
mwaka. Hata hivyo,

VITU VITATU HATARI ZAIDI
KATIKA SIGARA NI:

1. Tar: hiki ni kisababisha kansa katika mwili.

2. Nicotine: Hiki ni kitu chenye sumu ambacho
kwa muda mrefu sana kimetumiwa kama
dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya.
Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali
kabisa kwa athari yake mbaya katika mwili
wa binadamu.

3. Carbonmonoxide: Hii ni gesi
inayopatikana katika moshi wa sigara.
Madhara mbalimbali ya vitu vinayopatikana
katika moshi wa sigara ni kama yafuatayo:
1. Kuharibika kwa utando mlaini katika njia za
hewa: katika njia ambayo pumzi hupita kuna
kama tabaka fulani ambalo ni laini
limezunguka katika njia.
 Tabaka hili hufanyakazi ya kuzuia vumbi vumbi linaloingia
pamoja na hewa. Ile tabia ya uvutaji hufanya
vile vitu vinavyopatikana katika moshi wa
sigara kuganda katika utando huu na
kusababisha njia kuwa nyembamba kwa kule
kuongezeka kwa takataka na kemikali katika
njia, hivyo kumfanya mvutaji apate shida ya
pumzi hapo baadaye.

2. Vidonda vya tumbo: uvutaji wa sigara
huchochea utengenezaji wa acid ambayo
huweza kumletea mvutaji huyo vidonda vya
tumbo.

3. Matatizo katika mfumo wa upumuaji:
wavutaji hupata shida katika koo na mapafu
hivyo kupata kifua mara kwa mara na
maumivu na mwishowe kupata madhara
makubwa katika mfumo mzima wa upumuaji
kutokana na kuharibika kwa mapafu kama
tutakavyozungumzia katika pointi namba 7
hapo chini. Hali ya hewa huwaathiri sana
wavutaji sigara kwani hupata pneumonia na
asthma.

4. Udhaifu katika mifupa (Osteoporosis):
katika moshi kuna metali ijulikanayo kama
cadmium ambayo inaweza kusababisha
matatizo katika mifupa, hii husababisha
kupoteza asilimia 30 ya calcium katika mifupa.
Kwa wanawake uvutaji wa sigara
umeonekana kuzuia shughuli ya estrogen na
kitu chochote kinachozuia estrogen kufanya
kazi husababisha udhaifu katika mifupa
(Osteoporosis) na hii huweza kusababisha
maumivu ya mara kwa mara katika mifupa.

5. Kuwahi kumaliza kufikia mzunguko wa
mwezi (Menopause): Menopause ni ile hali ya
mwanamke kufikia mwisho wa mzunguko
wake wa kila mwezi ambao humpelekea
kushika ujauzito, hali hii huanza kutokea
akifikia umri wa miaka 45 – 55, hutofautiana.
wanawake wanaovuta sigara hufikia
menopause miaka mitano mapema zaidi ya
wasiovuta.

6. Athari kwa wenye mimba: wanawake
wanaovuta sigara huwa katika hatari kubwa
sana ya mtoto kutoka kabla ya siku zake
(Abortion) au kuua mtoto tumboni. Au hata
mtoto kufa mapema zaidi pindi
atakapozaliwa.

7. Kuharibika kwa Alveoli za mapafu
(Emphysema): ile harufu kali ya moshi
huharibu alveoli ndogo ndogo katika mapafu.
Hii kwa kiasi kikubwa sana hupunguza eneo
ambalo Oxygen hukutana na damu na hivyo
kusababisha hali inayoitwa Emphysema. Hali
hii hujitengeneza taratibu sana na kimya kwa
muda mrefu.
Wavutaji wote wana
Emphysema kwa kiwango fulani Lakini
kutokana na eneo kubwa wanaloishi ambalo
hupatikana Oxygen, watu wengi hawajui
kwamba wana hali hii. (watu wengi wana
takriban alveoli milioni 300 katika mapafu
yao) hivyo ni vigumu kugundua hali hii na
baadhi hujijua pale wanapofanya mazoezi
kwa mfano, na kuhisi ugumu wa pumzi.

8. Upungufu wa uwezo wa kubeba oxygen
katika damu: Carbon Monoxide (CO)
inapatikana katika moshi. Uhusiano wa
Carbon Monoxide kwa Haemoglobin ni
mkubwa mara 200 zaidi ya Oxygen. Hivyo
baadhi ya haemoglobin ya damu huzuiwa na
Carbon Monoxide kwa wavutaji kwani
haemoglobin badala ya kuchukua Oxygen
huenda katika Carbon Monoxide na hivyo
uwezo wa kubeba oxygen katika damu
hupungua.

9. Kansa/ Saratani: Katika asilimia kubwa ya
watu wenye kansa hupatikana kutoka kwa
wavutaji wa sigara, saratani za ngozi, koo,
utumbo, kibofu, mdomo n.k. vilevile saratani
ya figo, kongosho, tumbo na kizazi
imeonekana mara chache kwa wavutaji wa
sigara.

10.Kupungukiwa na vitamin: Uvutaji wa
sigara husababisha upungukiwaji wa Vitamin
hasahasa Vitamin C. ule uvutaji wa sigara
moja tu unaweza kupunguza kiasi cha
Vitamin C ambacho kinaweza kulingana na
ukubwa wa kutumia chungwa moja tu. Hivyo
inashauriwa kula sana Vitamin C ili
kurekebisha hali hii.

11. Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha
kisukari: Nicotine huchochea sukari katika
damu kwa kuilazimisha au kuichochea
Adrenaline na Non Adrenaline ambayo
hufanya ini na misuli kupeleka sukari katika
mishipa ya damu. Hii hufanya kongosho
ifanye kazi ya kutoa Insuli mara kwa mara ili
kudhibiti sukari kama kawaida yake na
kutokana na kufanya kazi huku mara kwa
mara hufanya kongosho ichoke haraka na
kushindwa tena kudhibiti sukari, hivyo
humsababishia mtu huyu kisukari.
Kwa upande wangu hizo ndizo athari
zinazotokana na uvutaji wa sigara, hivyo basi
jaribu kulinganisha yale manufaa ya muda
mfupi anayoyapata mvutaji na hasara zake.
Hapo utaona kwamba uvutaji wa sigara ni
hatari sana kwa afya yako, na ni bora ujitahidi
sana uache ili kuboresha afya yako
back to top