
Hili agizo limesikika kutoka kwa waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta wakati akijibu maswali bungeni Dodoma October 30 2013 baada ya kuulizwa uhalali wa Tanzania kuendelea kubaki kwenye Jumuiya hii wakati inatengwa na nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.
Waziri Sitta amesema wakati Tanzania inasubiri ufafanuzi wa hoja yake, itaendelea na msimamo wake wa kutoyatambua maamuzi yote yanayojadiliwa na kuamuliwa nje ya utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
‘Kama wenzetu hawa wana hila haitochukua muda tutazibaini tu lakini kwa kuwa sisi tumeshamuhoji mwenyekiti wetu wa baraza la Mawaziri na baada ya wiki mbili tuna kikao… basi tusubiri tutakachoambiwa, kama utaendelea uongo wa kitoto Serikali hii ni makini tutakuja bungeni kuweka mapendekezo yatakayokabiliana na hali ya kuchezewachezewa’ – Sitta

Mikutano ya nchi za Uganda, Kenya na Rwanda bila kuishirikisha Tanzania ilianza kufanyika Entebbe Uganda June 24 2013 ambapo mkutano wa pili ulifanyika August 28 2013 kwa kigezo cha kuzindua gati kwenye mji wa Mombasa nchini Kenya huku mwingine ukifanyika October 29 2013 Kigali Rwanda.
chanzo; http://millardayo.com