Baadhi ya wanafamilia wakiwa na nyuso za huzuni.
Mke wa Marehemu, Marry Kombe akiwa na simanzi msibani.
Baadhi ya waombolezaji wakipika chakula.
Kamera za GPL leo zilikuwa msibani eneo la Mtoni Kijichi Temeke
jijini Dar es Salaam kwa aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu, James
Kombe. Kamanda Kombe alifariki dunia jana katika Hospitali ya Ocean Road
jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu. Mwili wa marehemu
unatarajiwa kuagwa Ijumaa Oktoba 25 mwaka huu katika Kanisa la Lutherani
Msasani na baadaye kusafirishwa kuelekea Mwika mkoani Kilimanjaro kwa
mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi.
( GPL)