SURUALI YA MCHOMVU MH!

 
Mtangazaji wa kipindi cha XXL, Adam Mchomvu akiwa amevaa suruali yake iliyofananishwa na sketi.
SURUALI aliyovaa Mtangazaji wa Radio Clouds Fm, Adam Mchomvu wikiendi iliyopita pande za Ada State, Kinondoni, Dar iliwashangaza washikaji aliokuwa akipiga nao stori ambao waliifananisha na sketi.

Katika mazungumzo yao, ambayo yalinaswa paparazi wetu, marafiki zake walimshangaa kwa kujifanya mgumu wa Hip Hop huku akiwa amevaa suruali hiyo ambayo inabana miguu na kumwagika chini kama sketi (angalia picha).
Katika kujitetea, Mchomvu alisema: “Hii siyo sketi kama mnavyosema. Hii nguo ni mahususi kwa wale watu wenye kibusha lakini mimi nimevaa tu kama swaga fulani na wala siyo sketi,” alisema Mchomvu.
back to top