ODAMA NA HOFU YA KUMWANIKA MCHUMBA

MKALI wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ ameonesha kuwa ana hofu ya kumtangaza mchumba wake akidai anaogopa kukiuka tamaduni za Kitanzania.

 
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Akizungumza na Stori, Odama alisema japo anatamani kuwa kama wasanii wengine wanaoanika wachumba wao lakini bado anaona siyo jambo la busara wakati hana uhakika kama aliyenaye ndiye mume wake mtarajiwa au la.
“Nafikiri siyo sahihi kabisa kuanika uhusiano wa kimapenzi kwa watu mbalimbali wakati mtu huna uhakika na mpenzi uliyenaye kama atakuoa ama nini,” alisema Odama.
back to top