
Linah akipozi na mmoja wa wanaume walioomba kupiga naye picha.
Ijumaa limekuwa likimfuatilia Linah na kubaini kuwa kila mara hupenda
kuvaa nguo zinazoacha wazi mapaja na kitovu chake na watu ambao amekuwa
akipiga nao picha ni wanaume ambao wengi huonekana wakiwa wamemshika
kimahaba.
Linah akiwa jukwaani wakat wa shoo ya Fiesta 2013 jijini Dar.
Hata hivyo, licha ya mwenyewe mara kadhaa kueleza kuwa, hayo ni mvazi
ya kikazi zaidi, baadhi ya mashabiki wamemponda na kumtaka kubadilika
hasa ikifahamika kuwa ni mtoto aliyetokea kwenye familia iliyoshika dini
na kwamba kuvaa hivyo ni kujidhalilisha.