Dodoso hilo limeeleza kuwa Sera ya
Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango
cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini
Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini na mtihani wa mwisho
utachangia asilimia hamsini pia.
Mathalani, kwa mtihani wenye alama za jumla ya 100, mwanafunzi akipata alama 50 kupitia kazi za shule, atatakiwa kutafuta alama 50 katika mtihani wa mwisho.
Kwa kutumia mfumo huu, mwanafunzi atakuwa anakwenda kufanya mtihani akiwa tayari anajua alama za mchango wa kazi shuleni (continuous assessment) na kuwa na hakika ya anachotakiwa kukipata wakati anakwenda kufanya katika mtihani:

“Hatutaki
kuona mwanafunzi hanufaiki na kile alichokivuna akiwa shule. Mfano
mfumo wa sasa mwanafunzi aliyepata alama F ni aliyepata alama kati ya
0-34.
"Lakini hapo kuna wanafunzi ambao wamezidiana kwa mfano aliyepata
alama 20, hawezi kuwa sawa na aliyepata 0 ingawa wote wanawekwa kundi la
F,” alifafanua Profesa Bhalalusesa.
“Hata hivyo, kumekuwa na mitizamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi. Mfumo huu hata hivyo hautumiki kwa wanafunzi wa kujitegemea,” lilieleza dokezo hilo.