Malighafi za kiwanda zikiendelea kuteketea kwa moto kabla ya zimamoto kufika katika eneo la tukio.
Gari la kikosi cha zimamoto likiwasili eneo la tukio ili kuzima moto huo.
Moto umepungua baada ya kikosi cha zimamoto kufanya juhudi za kuuzima.
Leo Oktoba 24 majira ya saa 5 asubuhi, malighafi za kiwanda cha kutengeneza kandambili cha OK Plasctic Limited
zimeteketezwa kwa moto na mtu ambaye jina lake halikupatikana mara
moja. Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuuzima moto huo lakini tayari
malighafi nyingi zikiwa zimeshateketezwa kwa moto huo.
Aidha polisi
walijitahidi kumsaka na kufanikiwa kumtia mbaroni ambapo mpaka sasa
mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
(PICHA NA HABARI: MAKONGORO OGING' /GPL)