
UPARA
Nywele
ni sehemu katika mwili wa binadamu na hivyo zinatakiwa kupewa uangalizi
kama ambavyo sehemu nyingine za mwili zinavyopewa uangalizi.
Miaka ya
hivi karibuni, watu wengi wamekumbwa na matatizo ya kuwa na upara na
hususani kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 20 – 25. Watu wana
mitazamo tofauti kuhusu upara ( wapo wanaoamini upara ni ishara ya kuwa
na elimu sana au kuwa na busara sana), lakini leo napenda kukufahamisha
vitu kadhaa ambavyo vinaweza kumfanya mtu apate upara.
Mpenzi
msomaji, kitu cha kwanza kinachoweza kumfanya mtu apate upara ni
matumizi ya pombe katika umri mdogo. Utakumbuka kuwa bidhaa zenye kilevi
haziruhusiwi kuuzwa au kutumiwa na watu wenye umri chini ya miaka 18
kwa sheria za Tanzania. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kwa watu wenye
umri huu miili yao na mifumo mbalimbali katika mwili haijakomaa vizuri
na hivyo endapo kilevi itatumiwa, basi itaathiri ukuaji wa mtu
huyu ikiwemo swala la afya ya nywele zake.
Kitu cha
pili ni, ulaji wa nyama ambayo ilichakachuliwa kwa kumchoma mnyama
mfano ng’ombe sindano ili kumuongeza uzito .
Mtu kuwa
na upungufu wa vitamini D, hii imekuwa chanzo cha mtu kupuputika au
kunyonyoka nywele na mwinyowe kufikia hatua ya kupata upara.
Mtu
kuugua magonjwa sugu au kuwa na magonjwa yasababishwayo na virusi, hii huudhoofisha mwili na kupelekea nywele zinyonyoke.
Kwa
wanawake tatizo la upungufu wa damu, anaemia pamoja na matatizo katika
kizazi, Polycystic Ovary Syndrome (PCOS), imekuwa chanzo cha nywele
kunyonyoka, wanawake huwa na mabadiliko ya mala kwa mala ya homoni
mwilini, na baada ya kujifungua mtoto pia, homoni mwilini huwa haziko
imara vizuri na hivyo hukumbwa na tatizo hili.
Maisha
ya kukaa sehemu moja bila ya kujishughulisha na kitu au kazi, Sedentary
lifestyle, hii hupelekea mwili kuwa na mafuta au cholesterol nyingi
ambazo zinaongeza hatari ya kunyonyoka nywele na kupata upara.
Mpenzi
msomaji, kwa wapenzi na wafuatiliaji wa mambo ya mpira, watakumbuka
mchezaji wa mpira wa miguu katika timu ya Manchester United, Wayne
Rooney, alikuwa na tatizo hili, na njia aliyoitumia ni kufanyiwa
upandikizi wa nywele kwa gharama ambazo mtu wa
kawaida hawezi kuzimudu.
Tatizo
la nywele kunyonyoka linaweza kutatulika, njia mojawapo za kuepuka
tatizo hili ni kuepuka matumizi ya kilevi, kula chakula au kunywa
vinywaji ambavyo havijachakachuliwa, kujishughulisha au kufanya mazoezi
pamoja na kufuata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu namna ya
kuitunza afya yako.