MAKOSA 10 WANAUME HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA -5

 
MDAU wa safu hii, natumaini tangu nilipoanza ‘topiki’ hii umejifunza mambo ambayo yatakusaidia kuboresha uhusiano wenu wa kimapenzi. Hebu tuendelee sehemu hii ya tano...

 
 Staili yako ya maisha ni ya kiutu uzima zaidi, kwa hiyo unaona aibu kuzungumza maneno ya shombo faragha kama ambavyo vijana wa mjini hufanya. Hapo unakosea, tofautisha ulimwengu wa kawaida na ule wa ndani ya chumba, mkiwa wawili.
Pointi ya kwanza ni uhusika wenu. Mnakutana mkiwa hamna nguo, hiyo tu ikupe jawabu kwamba ulimwengu huo ni wa aina ya peke yenu. Kama hivyo ndivyo ilivyo, inakuwaje busara za barabarani au ofisini uzilete eneo hilo? Jiachie baba, maneno ya shombo yazungumze.
Wanawake pia hupendelea mapenzi yaliyo katika sura nyororo. Wenzako siku hizi wanasoma vitabu, wanaangalia tamthiliya kila siku, wanajionea uhusika wa kimapenzi katika sura tofautitofauti. Usisahau kuwa wengine hutazama mpaka pono, kwa hiyo wanajua aina mbalimbali za kile ambacho watu hutendeana kitandani.
Sikwambii uende ukanyanyue chuma ili ujaze kifua kama tembo au usuke nywele, uwe mtu wa kujipamba sana, la hasha! Ushauri wangu kwako unajikita kwenye eneo moja muhimu kwamba hakikisha hukosei mambo muhimu ambayo yanahitajika faragha.
BILA SHAKA UMEELEWA
Usikariri staili, leo umeanza katikati, kesho anza juu kushuka chini. Siku nyingine pointi yako ianzie chini kwenda juu. Jitahidi usiwe yuleyule siku zote, atakuzoea na atakuchoka. Mapenzi hayana mfumo maalum, kinachoangaliwa ni wewe na yeye kufurahia tendo.
Hautaonekana mjinga kama kuna siku utapita njia za panya, hakuna ‘romansi’ wala nini, mradi umehakikisha njia imeshakuwa vizuri. Usijipe sifa ya ushamba ambayo hauna. Unaweza kabisa, wewe ndiye mwanaume bora kuliko wote duniani, kwa hiyo tumia uwezo ulio ndani yako.
KUJISAHAU KUWA WEWE NI MWANAUME
Waulize wanawake 100 swali hili kwamba wangependa mwanaume wa aina gani kitandani? 99 kati yao, jibu lao litakuwa wazi kuwa wanahitaji mwanaume ambaye atakuwa kiongozi faragha. Hawataki yule anayekwenda kama zezeta halafu anaelekezwa cha kufanya kila hatua.
Ni ukweli kwamba wanawake huendesha harakati za haki sawa lakini kwenye maeneo mengi huhitaji watendewe zaidi. Mojawapo ya mambo hayo ni hili la faragha. Asikwambie mtu, hakuna mwanamke anayetaka yeye ndiye awe kiongozi, eti amuongoze mwanaume cha kufanya.
Isipokuwa, mwanamke kwa uhusika wake, hujituliza kama kifaranga cha kuku kwa mwanaume. Sasa basi, unatakiwa ulijue hilo, siyo unaulizauliza maswali au unaingia faragha kisha unabaki kushangaashangaa, unatakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye utekelezaji halafu yeye afuate.
Kuna mwanaume yupo kitandani lakini anajikausha eti anasubiri mwanamke ndiye aanze kumchokoza. Wewe wa wapi? Chukua nafasi yako kama kiongozi, kwa hiyo anzisha mwendo na nyakati zote simama kwenye uhusika wako. Usipende kubembelezwa, hiyo siyo sifa ya kiume.
Haina maana kwa sababu nimekwambia usimame kama mwanaume ndiyo sasa ugeuke mbabe, umshike mwanamke na umtenge katika mtindo unaotaka pasipo kujadiliana naye, hapana, hapo utakuwa unakosea kabisa. Ukifanya hivyo utakuwa unakwenda nje ya ukweli.
Mantiki hapa ni kukutaka uongoze kwa kufuata demokrasia. Usimpelekeshe isipokuwa shauriana naye halafu mkubaliane kumfanyia kile ambacho anataka. Ukiwa hivyo, siku zote mwanamke wako atakuona wa kipekee. Hutamchosha na atakapokuwa anafikiria haja zake za faragha, wewe ndiye utakayetawala hisia zake.
Ogopa sana ukiwa na mwenzi wako halafu hisia zake zinakuwa za kuibiaibia au akawa anachukia mapenzi kabisa. Hapo picha ya haraka ije kwenye fikra zako kwamba wewe ni tatizo, kwamba umekuwa ukimhudumia ndivyo sivyo mpaka umemsababishia apoteze hamu ya mapenzi.
Itaendelea wiki ijayo.
back to top