Unalizungumziaje suala la nguo fupi kwenye filamu?
Moja ya mambo yanayojadiliwa sana na vyombo vya
habari kwa sasa, ni suala la kina dada wa bongo movies kupenda kuvaa
nguo fupi sana wanapokuwa wanaigiza filamu zetu hizi. Ikizingatiwa ni
karibuni tu, suala hili lilijadiliwa mpaka bungeni na pia siku chache
zilizopita mwigizaji maarufu nchini Simon Mwakifamba aliongea na chombo
kimoja cha televisheni na kusema kuwa wadada hawa lengo lao ni kuonesha
miili yao kwa lengo la kujiuza,
sisi tukiwa kama tovuti rasmi ya filamu
Tanzania tungependa kupata maoni yako wewe mdau na mpenzi wa tasnia yetu
hii, Je, wewe unalichukuliaje suala hili? Ni kweli haya madai yana
maana na inabidi yafanyiwe kazi au wanafanya hivyo kama sehemu ya sanaa?
Tupe maoni yako hapo chini mdau.