Neymar siku aliyotambulishwa kama mchezaji wa Barca.
Kiungo mshambuliaji wa Fc Barcelona Neymar Da Silva Jr amelipa fedha
ambayo mabingwa hao wa Hispania walitumia kumnunua kabla hata ya
kuichezea timu hiyo kwenye mchezo wa ushindani .
Barcelona imeshuhudia mauzo ya jezi 570,000 zenye jina la Neymar
yakilipa euro milioni 57 ambazo Barca ilizilipa kwa klabu ya Santos
kumnunua star huyo wa Brazil.
Mashabiki wa Barca wakionyesha Jezi ya Neymar.
Hadi sasa Barcelona imeuza jezi laki tano na elfu sabini kwa bei ya
euro mia moja kwa kila jezi hali inayofanya hela iliyotumika kumsajili
Neymar kurudi haraka kabla hata ya msimu kuanza .
Kwa mahesabu ya haraka haraka jezi 570,000 x Euro 100 inakupa jibu la
57,000,000 ambayo Barcelona ililipa Santos kumnunua Neymar .
Jezi ya Neymar ambayo hadi leo zaidi ya mashabiki laki tano wameinunua kwa bei ya Euro 100.
Hadi sasa Neymar ameiwakilisha Barcelona kwenye mechi mbili pekee
akiwa amefunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya timu ya Thailand na mauzo
ya jezi