MTANZANIA MWINGINE AKAMATWA HONG KONG NA MADAWA YA KULEVYA YAKIWA NDANI YA MASHINE ..!!
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege
wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea
Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.Dawa
hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla
zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa
hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza
dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha
mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo
na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.