
United ilifunga mabao yake kupitia kwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu uliopita Robon Van Persie ambaye alifunga mabao yote mawili .
United iliingia kwenye mchezo huo bila mshambuliaji wake Wayne Rooney ambaye hakuchaguliwa kwa kuwa ni majeruhi huku mustakabali wake ndani ya klabu hiyo ukibakia kuwa kitendawili .

Taji la Ngao ya Jamii linakuwa taji la kwanza kwa kocha mpya David Moyes tangu alipoteuliwa kurithi nafasi ya kocha wa zamani Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu wa ligi ulioisha .
David Moyes ataanza rasmi kampeni ya utetezi wa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa klabu yake wiki ijayo wakati Manchester United watakapovaana na Swansea City kwenye mhezo wao wa kwanza wa ligi .