
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa upande wa
utetezi, Peter Kibatala kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo iliposomwa
Julai 3, mwaka huu kwa madai ya kuwa hati ya mashtaka ni dhaifu kisheria
na haionyeshi ni makosa yapi mtuhumiwa aliyotenda.
Wakili Kibatala alieleza mahakama kuwa kifungu cha
129 na 132 cha sheria ya mwenendo wa makosa jinai ni lazima mshtakiwa
aelezwe mashtaka yake wazi wazi yanayomkabili.
Murji alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akikabiliwa na kesi ya uchochezi anayodaiwa kuifanya Januari 19,mwaka huu katika eneo la Ligula mkoani hapa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Dynes Lyimo alifuta shtaka hilo na kumwachia mshtakiwa huru baada ya kesi hiyo kuahirishwa tangu Julai 3,mwaka huu.
Wakati huo huo viongozi wa upinzani Katani Ahmed Katani (33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF wanaokabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamhuri wamefikishwa mahakamani.