
Omotola
IMEKUWA ni jambo la kawaida kabisa kuona ndoa za mastaa
zikivunjika. Kashfa za ufuska pamoja na nyingine kadha wa kadha zimekuwa
zikitajwa kama sababu za kusambaratika kwa ndoa hizo.
Pamoja na kuwako kwa idadi kubwa ya ndoa za mastaa
zinazovunjika, wapo wengine ambao ndoa zao zimekuwa mfano mzuri,
unapenda kuwafahamu?
Joke Silva
Ndoa ya mwigizaji Joke Silva ni miongoni mwa ndoa chache za Nollywood zilizoweza kukaa kwenye mstari bila ya mgogoro.
Tofauti na ndoa nyingine za Nollywood, ya kwake
imeishi kwa kipindi kirefu bila kuwa na kashfa. Mume wa mwigizaji huyu,
Olu Jacobs, ni nguli wa maigizo.
Ndoa yao inatajwa kuwa iliyojawa na furaha na
baraka tele. Ndoa hiyo kwa sasa ina miongo mitatu na sasa Joke
anaonekana kama kioo kwa wanawake wengi Nigeria hususan vijana.
Henrieta Kosoko
Ndoa ya Henrietta Kosoko nayo pia inatajwa kuwa ya
mfano. Licha ya kuwa kwenye ukewenza lakini bado inaonekana kuwa ni
ndoa imara kiasi cha kuhusudiwa na watu wengi. Siku zote amekuwa
mwaminifu si tu kwa mumewe bali hata kwa jamii inayomzunguka jambo
linalochangia kuiweka ndoa hiyo kwenye mstari ulio sawa.
Ngozie Orji
Ngozie Orji, mke wa mwigizaji, Zack Orji, naye anatazamwa kama kioo. Ndoa yao imedumu kwa muda wa miongo miwili sasa.
Katika kipindi hicho wamejaliwa kupata watoto
watatu. Kwa Nollywood ndoa yao inatajwa kuwa miongoni mwa ndoa zenye
mafanikio makubwa sana.