KWELI Waswahili usema kua uyaone, awali nilifikiri mjini ni maghorofa
kumbe ni zaidi ya hayo maghorofa, hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu
kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva kupekuliwa
Airport, wasanii wa muziki huu kwa sasa si marafiki wa viwanja vya Ndege
swali linakuja je wasanii wa filamu nao watapata jeraha hilo?
Wema Sepetu mwigizaji wa filamu Swahilihood
Madee mmoja wa wasanii aliyekutana na sakata Airport.
Kufuatia kashifa ya uvushwaji wa madawa ya kulevya inayolisakama Taifa la Tanzania wasanii wa muziki wa Bongo fleva wamekuwa waathirika wakubwa katika viwanja vya Ndege kwani inapofikiwa wakati wa kupekuliwa wanapekuliwa kweli kweli hadi wengine wanakasirika na kuhisi kama wanadharirishwa kwa kufanyiwa hivyo.
Wabongofleva ambao moja kwa moja wameonja adha ya kuhisi wanaweza kuwa na Ngada katika mabegi yao ni pamoja na Ambwene Yesaya AY ambaye alikutana na mkasa huo akiwa uwanja wa ndege na kutumia muda mwingi katika kupekuliwa hadi pale waliporidhika na kuona hana hatia na kuruhusiwa kuendelea na safari yake baada ya kujiridhisha.

Wolper Gambe msanii wa filamu Bongo.
AY mwanamuziki wa Bongofleva
Naye Raisi wa Manzese Hamad Ali aka Madee alikutana na kimbembe pale alipotua nchini Afrika ya kusini akiwa sambamba na Mzimbabwe wao pekee ndio waliowekwa kiti moto kwa kupekuliwa zaidi ya saa moja kwa kuvuliwa hadi nguo za nyepesi za ndani na mabegi yao kwa kumwaga nguo zote na baadae kuombwa radhi kwa muda wao na kupekuliwa sana.
Sasa watu wanajiuliza kuwa je hali hiyo kwa upande wa wasanii wa Bongo Movie nao wanaweza kukutwa na adha hiyo ? ya kupekuliwa hadi kutumia zaidi ya muda mrefu hata kudharirishwa kwa kukaribia kuvuliwa kufuli, hakuna anayejua kuhusu hilo kwani wengi wanaamini kuwa inawezekana kwa sababu wanasafiri sana tofauti na waigizaji maswali ni mengi.
Pengine historia nayo inachangia hadi leo kwa wasanii wa filamu
hakuna taarifa sahihi kuhusu kashifa ya matumizi ya madawa ya kulevya
kwa waigizaji jambo ambalo limekuwa likiripotiwa kila siku kwa wasanii
wa Bongo fleva pamoja na watu wao wa karibu kama wapenzi wao na Video
queen ambao tayari wamekamatwa na madawa ya kulevya.
Sakata lilianzia pale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye
kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea
Tanzania,.
