Huu ndio ugunduzi mpya unao-make headlines kwenye sekta ya usafirishaji hivi sasa

large
Ugunduzi mpya ambao una-make headlines hivi sasa ni wa bilionea Elon Musk ambaye pia alikuwa ni mmoja kati ya watu waliotengeneza mfumo wa malipo kwenye mtandao “Paypal”. Hyperloop utaongeza aina ya nne ya usafiri baada ya anga,majini,barabara na treni. Hyperloop usipo angalia vizuri unaweza kusema ni train za umeme lakini ni aina tofauti kabisa na zina kasi ya ajabu.

Njia ya Hyperloop inajengwa  yard 50 hadi 100 kutoka kwenye ardhi na huko juu ndiko Hyperloop zitapita kama zinavyoonekana kwenye picha hapo juu. Unaambiwa Hyperloop inauwezo wa kwenda km 900 kwa saa hadi km 1000 kwa saa. Elon Musk ametoa design ya kwanza ya njia ya kutoka Los Angels hadi San Fransisco ambayo ni km 570 ambapo safari inakamilika ndani ya dakika 35 na abiria mmoja kulipia dola 20.
Bajeti ya kutengeneza mfumo huu unagharimu dola bilioni 5 kwa ajili ya mfumo utakaobeba abiria na mizigo tu, ili mfumo huu uweze kubeba na magari ya abiria itahitajika bilioni 2.5 za ziada. Sehemu kubwa ya mradi huu unategemewa kutumia umeme wa Solar system. Soma zaidi kuhusu Hyperloop HAPA
Sekta ya usafirishaji ni muhimu sana ambapo bado wachunguzi wengi wanajaribu kuja na njia tofauti za usafirishaji ambazo zitatumia gharama ndogo.
hyperloop-tubing
Mchoro wa Hyperloop kama unavyoona Solar panel ambazo ni chanzo kikubwa cha umeme kwenye huu mfumo
tunnel-transport
musk-developing-hyperloop-demonstrator-5
back to top